Jermain Defoe atua Sunderland

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Colin Defoe

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingereza Jermain Colin Defoe amejiunga na timu ya Sunderland.

Defoe mwenye miaka 32 aliekua akiichezea timu ya Toronto FC ya nchi Marekani amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu kuweza kuitumikia timu hiyo.

Mshambuliaji huyu mwenye uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu alijiunga na Toronto akitokea klabu ya Tottenham alikocheza kwa mafanikio makubwa .

Alifunga Zaidi ya magoli 120 katika ligi England akiwa anazitumikia timu za West Ham United, Portsmouth and Tottenham Hotspur.

Mshambuliaji Sunderland Jozy Altidore, amepelekwa kwenye timu ya Toronto kama sehemu ya makubaliano ya uhamisho huo.