Heather Watson atinga fainali

Image caption Furaha ya ushindi ya Heather Watson

Mcheza tenesi Heather Watson amefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michezo kimataifa ya Hobart.

Watson amemshinda mpinzani wake Alison Riske kwa kuchapa kwa jumla ya seti 6-3 na 7-5.

kwa ushindi huu nyota huyu wa tenesi anasubiri kucheza fainali na mshindi kati ya Madison Brengle na Mjapani Kurumi Nara.

"Nina furaha hatimae nimefika hapa siku ya leo, ulikua ni mchezo mgumu," alieleza Watson

Baada ya mchezo wa fainali siku ya jumamosi mcheza tenesi huyo ataelekea nchini Australian kwenye michuano ya wazi ya Melbourne.