Simeone:Torres Mwanaume

Haki miliki ya picha epa
Image caption Ni mara ya kwanza Torres kuifungia Atletico Madrid tangu ajiunge nayo

Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone amesema Fernando Torres amerejea kuwa ''mwanaume'' ndivyo alivyomuita hivyo baada ya mshambuliaji huyo kufunga magoli yake ya kwanza tangu alipojiunga na Atletico madrid.

Mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Torres alijiunga na Liverpool mwaka 2007.

Torres alijiunga na Atletico mwanzoni mwa mwezi huu na aliifungia klabu hiyo magoli mawili katika dimba la Bernabeo na kutoka sare ya mabao 2-2 ilipokutana na Real Madrid katika michuano ya Copa del rey

Torres naye ameonesha furaha yake na kushukuru wapenzi wake kwa kumuunga mkono.