Viwanjani mwishoni mwa wiki

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Olivier na tabasamu la ushindi

Ligi kuu ya England imeendelea kwa mechi mbili ambapo..Arsenal imeibamiza Man City ,Huku Westham Ikiibamiza Hull City bao 3-0

Nayo Michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika ikiwa imeng'oa nanga hapo jana kwa Gabon Kuilaza Burkina faso bao 2-0 Huku Pierre Emerick Aubemeyang aking'ara vilivyo.Nao wenyeji Equitorial Guinea wakishikwa shati na Congo Brazaville kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1.

Ligi kuu ya England ambapo Jumapili zimechezwa mechi mbili ,Katika mechi ya awali Westham United iliibamiza Hull City bao 3-0 mabao yaliyotiwa kambani na Andy Carrol katika dakika ya 49,Amalfitano katika dakika ya 69 na Stewart Downing aliyehitiisha ushindi huo mnono wa Westham katika ya 72 akimalizia pasi murua ya kiungo Mcameroun aliyeko kwenye Fomu Alexandre Song.

Kwa matokeo hayo Westham imefikisha Point 36 wakiwa nafasi ya 7,wakiwa pointi moja mbele ya Liverpool wenye pointi 35 walioko nafasi ya 8,huku timu hizo zikitaraji kukutana katika mechi ijayo.

Na Tukielekea nchini Equatorial Guinea kwenye Michuno ya soka Kombe la mataifa barani Afrika iliyong'oa nanga hapo jana Jumapili zilichezwa mechi mbili ambapo katika Mechi ya Kwanza Zambia imeshuka dimbani kukabiliana na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika mechi ambayo Matokeo Yamekuwa bao 1-1 huku Zambia ikianza Kupata bao la kuongoza dakika ya 2 kupitia kwa Given Singuluma lililodumu hadi Mapumziko lakini baadae Wacongoman wakaweza kusawazisha katika dakika ya 66 kupitiwa kwa Mwanandinga Yanick Bollasie anayesukuma ngozi kwenye klabu ya Crystal Place nchini England katika dakika ya 66.

Katika mechi ya ufunguzi wenyeji Equatorial Guinea walinyang'anywa tonge mdomoni baada ya Congo Brazaville kusawazisha katika dakika ya 87 kupitia kwa Bofouma Koulousa aliyesawazisha bao na Nsue Lopez aliyeanza kuingia kambani mwa Congo katika dakika ya 16.

Na katika mechi ya pili Gabon waliwashangaza washindi wa pili wa Fainali zilizopita Burkinafaso kwa kuwalaza bao 2-0 huku Mshambuliaji Pierre Emerick Aubemeyang akitia kambani bao moja dakika ya 19, na kutengeneza bao la pili lililowekwa kimiani na Evouna Lengoualama katika dakika ya 72.

Katika Mechi ya pili baadae majira ya saa nne usiku kwa saa Afrika Mashariki Tunisia itashuka Dimbani kuwakabili Cape Verde katika Mechi ya pili ya Kundi B,

Shughuli kubwa inataraji kuonekana hapo kesho kwa mbili za kukata na shoka kwenye kundi C linalotajwa kama kundi la kifo la Kifo pale Black Stars ya Ghana itakaposhuka Dimbani kuwakabili Senegal huku Desert Warriors Algeria ikipambana na Afrika Kusini