Algeria yainyuka Afrika Kusini 3-1

Haki miliki ya picha AP
Image caption Timu ya soka ya Algeria

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon imeendelea nchini Equatorial Guinea, ambapo timu za kundi C zilipambana kusaka pointi tatu muhimu katika kuendelea na kinyang'anyiro cha taji la michuano hiyo.Timu ya Algeria, walionyesha ubora wao katika kusakata kabumbu, pale walipowachakaza Afrika Kusini mabao 3-1.

Afrika Kusini ndiyo iliyoanza kuliona lango la Algeria katika dakika ya 51 likifungwa na Phala. Algeria ilisawazisha bao hilo kwa mpira aliojifunga Thulani Hlatshwayo katika dakika ya 67, huku Ghoulam na Sliman wakifunga katika dakika ya 72 na 83 kama wanavyofuatana.

Algeria inashika nafasi ya 18 ya ubora katika viwango vya Fifa wakati Afrika Kusini ni ya 52. Kikosi cha Afrika Kusini chenye wachezaji 23, 18 kati yao wanacheza ligi ya ndani ya nchi yao.

Afrika Kusini pia ilikosa goli la penalti kupitia kwa Tokelo Rantie. Na endapo angepata mkwaju huo wa penalti Afrika Kusini ingeoongoza kwa mabao 2-0. Hata hivyo hiyo imebakia katika kumbukumbu tu za mchezo huo.

Mchezo wa mapema hiyo jana usiku, ulizikutanisha timu za Ghana na Senegal, ambapo Senegal iliibuka na ushndi wa mabao 2-1. Kama ilivyokuwa kwa Afrika Kusini, Ghana ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuona lango la Senegal kwa mkwaju wa penalti uliofungwa na Andre Ayew dakika ya 14. Hadi mapumziko Ghana ilikuwa mbele kwa bao hilo. Senegal ilibadilika na kuweza kusawazisha dakika ya 58 kupitia kwa mchezaji wake Mame Diouf. Mpambano huo ukionekana kumalizika kwa sare ya 1-1, mchezaji Sow alibadili matokeo kwa kufunga bao katika dakika ya 90 na kuiwezesha Senegal kuibuka mshindi wa mechi hiyo.

Katika kundi C, Algeria na Senegal zina pointi tatu kila moja, huku Ghana na Afrika Kusini zikibakia bila pointi.

Leo ni heka heka kwa kundi D lenye timu za Ivory Coast, Mali, Cameroon na Guinea. Mchezo wa kwanza utazipambanisha Ivory Coast na Guinea, baadaye watafuatiwa na Mali wakimenyana na Cameroon.

Habari nyingine za kimchezo zinamhusu mchezaji mahiri wa Ghana Asamoah Gyan. Mchezaji huyo ana matumaini atashiriki katika mchezo unaofuata kwa timu yake baada ya kukosa mchezo dhidi ya Senegal, kutokana na kuumwa malaria.

Anasema "wamesikitishwa na matokeo ya kufungwa 2-1 na Senegal. Anasema alifikiria wangetumia uzoefu wao". "walitushinikiza, walidhibiti mchezo daki 30 za mwisho na tungelazimisha sare. Lakini tulipoteza umakini na kufungwa goli dakika ya mwisho ya mchezo.

"Nilikuwepo kuipa moyo timu yangu- na tumepoteza leo. Sasa najisikia nafuu- Nazungumza na jopo la madaktari na tutaona kitakachotokea." Ni kauli ya Asamoah Gyana ambaye alikuwa akisumbuliwa na malaria na kukosa mechi ya kwanza kwa timu yake ya Ghana.

Timu ya Algeria, walionyesha ubora wao katika kusakata kabumbu, pale walipowachakaza Afrika Kusini mabao 3-1.