Senegal vs Ghana:Ukweli wa mambo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Diafra Sako

Tangu mwaka 2008 Ghana imepoteza mechi moja kati ya 11 katika makundi ya mechi za mataifa ya afrika.

Timu hiyo kwa jina the Black stars imecheza bila kushindwa katika mechi zake kumi za makundi.Senegal nayo imecheza mechi 11 huku ikipoteza kadhaa na kudhina nyengine.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Gyan

Hatahivyo timu hiyo ya Simba wa Teranga imefunga katika mechi tisa kati ya 10.

Simba hao wa Teranga wameshindwa kushinda michuano mitatu ya mechi za kombe la mataifa ya afrika dhidi ya Ghana.