Andy Murray aanza kwa ushindi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Andy Murray

Mcheza tenesi Andy Murray ameanza michuano ya wazi ya Melbourne,kwa ushindi baada ya kumchapa Yuki Bhambri.

Murray ameanza kwa ushindi huo kwa kushinda seti 6-3 6-4 7-6 (7-3) katika mchezo uliotumia saa na dakika kumi na mbili katika uwanja wa Margaret Court.

Murray mwenye miaka 27, alianza kwa kupoteza seti ya kwanza kwa kuchapwa 4-1 kabla ya kurudi na kufanikiwa kuibuka mshindi.

"Nafikiri ni mwanzo mzuri, mpinzani wangu alicheza vizuri na kushambulia vizur katika mchezo wote.

Yuki Bhambri ameweza kutoa upinzani wa kutosha kwa Murray japo kuwa yuko chini sana katika viwango vya tenesi akishika nafasi ya 317 katika ubora wa dunia .

Murray atakabiliana na Marinko Matosevic wa Australia katika mchezo unaofuata siku ya Jumatano.

Huku nyota mwingine wa tenesi Rafael Nadal nae akimshinda Mikhail Youzhny,

Nadal ameshinda kwa 6-3 6-2 6-2 katika mchezo wake wa kwanza toka alipokosa michezo ya Wimbledon kutokana na kuwa majeruhi.

Kwa upande wa wanawake Ana Ivanovic alishangazwa na Lucie Hradecka Jamuhuri ya Czech.kwa kukubali kuchapwa 1-6 6-3 6-2 .