Ivory Coast yatoka sare na Guinea

Haki miliki ya picha AP
Image caption ivory Coast

Ivory Coast imepata sare ya moja kwa moja dhidi ya Guinea katika kombe la mataifa ya Afrika baada ya Guinea kuwa wa kwanza kupata bao licha ya mshambuliaji Gervinho kupewa kadi nyekundu.

Guinea ilichukua uongozi kunako dakika ya 36 baada ya Mohammed Yattara kucheka na wavu.

Aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal Gervinho ambaye mkwaju wake ulipiga mwamba wa goli la Guinea katika kipindi cha kwanza alipewa kadi nyekundu na hivyobasi kutoka nje katika dakika ya 58.

Mcheza Traore wa Guinea karibia apate bao la pili wakati kombora lake lilipogonga mwamba wa goli,lakini IvorY Coast ilijiokoa baada ya Seydou Doumbia Kufunga katika eneo la hatari.