Michuano ya kombe la Capital One

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raheem Sterling

Raheem Sterling aliihakikishia Liverpool kucheza nusu fainali za kombe la Capital One huku Chelsea ikibakia vizuri baada ya bao la penalti la Eden Hazard wa Chelsea katika dakika ya 18 kurejeshwa na Sterling katika dakika ya 59.

Chelsea ilipatiwa penalti baada ya Emre Can kumchezea vibaya Hazard.

Hata hivyo, Sterling aliipatia Liverpool bao ililostahili katika mchezo wa kwanza uwanja wake wa nyumbani wa Anfield.

Timu hizo zinarudiana Jumanne, tarehe 27 Januari, 2015.