Equatorial Guinea , Burkina Faso kivumbi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Equatorial Guinea dhidi ya Burkina Faso na Gabon na Congo kukipiga leo

Mzunguko wa pili wa michezo ya michuano ya kombe la Afrika itaendelea tena kwa wenyeji Ikweta kujitupa uwanjani kucheza na Burkina Faso.

Mchezo huu utapigwa kwenye dimba la bata, Nahodha wa Burkina Faso Charles Kabore amesisitiza watafanya vizuri baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Gabon.

"Mashindano hayajafika mwisho kwetu,tunatakiwa kushinda dhidi ya wenyeji na kila kitu kitakua sawa kwetu."

Esteban Becker kocha wa Guinea ya Ikweta anajua timu yake iko kwenye wasiwasi mkubwa kutokana na kushindwa kushinda mchezo wa kwanza.

Mchezo wa pili utawakutanisha Gabon na Congo ambapo pia utapigwa kwenye dimba la Bata,

Gabon wanaongoza kundi A wakiwa na pointi 3 baada ya kuwachapa Burkina Faso, ikiwa watashinda mchezo huu watakua wamejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya mtoano.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Uwanja ambako michuano ya Afcon inashindaniwa

Nahodha wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang ataendelea kuaminiwa katika kulisaidia taifa lake ili kufuzu kwenye hatua ya mtoano.

Kwa upande wa Congo ambao walianza kwa sare ya kufungana moja moja na Guinea ya Ikweta watakua na kibarua kizito kuweza kuibuka na ushindi.

Kocha mkongwe Claude le Roy anatarajiwa kutumia uzoefu wake kwenye michuano hiyo kuweza kuisaidia timu yake

Roy amewahi kufanikiwa kuingia mara sita katika hatua ya nane bora katika michuno timu akiwa kocha wa mataifa tofauti.