Murray,Sharapova waendeleza ushindi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mcheza Tenisi Nyota,Maria Sharapova

Nyota wa Tenesi Andy Murray ameendeleza wimbi ushindi katika michuano ya wazi ya Melbourne.

Murray alimchapa Marinko Matosevic kwa seti 6-1, 6-3, 6-2 katika mchezo uliochezwa kwa muda saa moja na dakika 42.

"Nilianza vizuri mchezo, Mariko alikua taratibu kidogo mwanzoni lakini alikuwa anafanya vizuri kadri tulivyokua tunaendelea ulikua ni mchezo mgumu katika seti ya pili na ya tatu”.

Mchezo wa raundi inayofuata atacheza na Joao Sousa raia wa Ureno anayeshika nafasi ya 52 katika ubora wa tenesi

Kwa upande wa wanawake Maria Sharapova aliibuka kidedea kwa kumchapa Alexandra Panova 6-1 4-6 7-5.Sharapova atacheza na Zarina Diyas wa Kazakhstan au Anna Schmiedlova wa Slovakia