Cape Verde kumenyana na Congo DRC

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Afcon

Mkufunzi wa timu ya Cape Verde Rui Aguas amebaini kwamba atafanya mabadiliko katika mechi dhidi ya Congo DRC lakini akongezea kwamba ameamua kuweka siri mbinu atakayotumia.

Huku akikiri kwamba baadhi ya wachezaji wake wana majeraha amesema hatasema ni wachezaji gani.

Naye mshambuliaji wa DRC Congo Yannick Bolassie ambaye ndiye mfungaji wa bao lililosabbisha sare ya 1-1 dhidi ya Zambia anasema wataibuka washindi.

Amesema: Cape Verde ina wachezaji wazuri lakini tunataka kusonga mbele katika kundi hili halafu chochote chaweza kutokea''