Ebola:Mashabiki watakiwa kuwa na subra

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kolo Toure

Mlinzi wa Ivory Coast Kolo Toure amewataka mashabiki katika michuano ya mataifa ya Afrika nchini Equitorial Guinea kuwa na Subra wanapokaguliwa ugonjwa wa Ebola.

Mashabiki na maafisa wa polisi wamekuwa wakikabiliana kabla ya mechi kadhaa baada ya kucheleweshwa kutokana na upimaji wa Ebola nje ya viwanja vya soka.

''Nadhani mashabiki wanafaa kujua kwamba ni lazima wakaguliwa'' alisema mchezaji huyo wa liverpool.

Image caption Maafisa wa afya wakiwakagua mashabiki katika michuano ya Afcon

''Ebola ipo na watu wengi huwa hawaamini wanapofika katika maeneo ambayo hayana watu walioambukiwa''.aliongezea.

Wafanyikazi wa Shirika la afya duniani WHO,ambao wanafanya ukaguzi huo wa Ebola wanakutana alhamisi ili kujadiliana kuhusu wasiwasi wa usalama wao baada ya kukabiliana na mashabiki wengine nchini humo.