Serena,Novak Djokovic kidedea Melbourne.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Novak Djokovic

Serena William na Novak Djokovic wamefanikiwa kuingia raundi ya tatu ya michuano ya wazi ya Melbourne.

Serena aliibuka kidedea katika mchezo huo kwa kumchapa mpinzani wake Vera Zvonareva raia wa Urusi kwa seti 7-5 6-0.

Kwa upande wa wanaume Novak Djokov alimgaragaza vibaya Andrey Kuznetsov kwa kumchapa seti 6-0 6-1 6-4.

Bigwa mtetezi wa michuano hii Stan Wawrinka alimfunga Marius Copil kwa seti 7-6 (7-4) 7-6 (7-4) 6-3.