Tunisia yaizima Zambia

Haki miliki ya picha
Image caption Wachezaji wa Tunisia

Tunisia ilichukua fursa ya kushindwa kwa Zambia kufunga mabao ya wazi ilipotoka nyuma na kuishinda miamba hiyo ya Chipolopolo 2-1.

Mchezaji Emmanuel Mayuka alifungua ukurasa wa mabao katika mchuano huo baada kufunga krosi iliopigwa na Rainford Kalaba.

Lakini Mayuka alipata jeraha na hivyobasi kutolewa alipojaribu kufunga bao la pili alipokuwa amesalia na wavu.Lakini Ahmed Akaichi alisawazisha katika eneo la hatari.

Tunisia iliimarisha mchezo wake baada ya bao hilo na ilipofikia dakika ya 88 Yasine Chikhaoui alifunga bao la pili kupitia kichwa.

Tunisia sasa ina alama 4 baada ya mechi mbili huku Zambia ikiwa na alama moja huku kukiwa kumesalia na mechi moja katika kundi B la michuano ya mataifa ya Afrika.