Tunisia kutoana jasho na Zambia

Image caption Afcon

Zambia italazimika kuimarisha safu ya kati katika mechi didi ya Tunisia kufuatia jeraha la mchezaji Nathan Sinkala ambalo limemuweka nje ya michuano yote ya mataifa ya Afrika.

Hatahivyo kikosi hicho cha Chipolopolo hakina tatizo kubwa juu wachezaji wake.

Mkufunzi wa Tunisia ana wachezaji wa kutosha wa kujumuisha katika timu yake,ijapokuwa wamekuwa na tatizo katika hoteli yao.

Kunako mwendo wa saa nane leo alfajiri ,kulikuwa na maji chungu nzima katika vyumba vya hoteli wanaolala wachezaji wa kikosi hicho.

Inadaiwa kuwa wachezaji hao walilazimika kubadili vyumba huku wachezaji wengine wakilazimika kulala wanne katika chumba kimoja.