Real Madrid yamsajili Martin Odegaard

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Martin Odegaard

Miamba wa soka wa Hispania klabu ya Real Madrid imefika makubaliano ya kumsajili mshambuliaji kinda Martin Odegaard toka Stromsgodset.

Odegaard mwenye umri wa miaka 16 atatambulishwa mbele ya waandisha wa habari leo,Real Madrid haijaeleza imetoa kiasi gani cha fedha ili kupata saini ya kinda huyo.

japo vyombo vya habari vya Hispania vinasema wametumia kiasi cha euro milioni 3 kuweza kumpata mshambuliaji huyo.

Kinda huyo alieanza kuichezea timu ya Norway, akiwa na miaka 15 amekuwa akiwaniwa na vilabu kadhaa vikubwa barani ulaya,

Odegaard alifunga mabao 5 na kutoa pasi 7 za mabao katika michezo 23,aliyoitumikia timu yake ya Stromsgodset.

Mchezaji huyu anaetumia mguu wa kushoto anafananishwa na Lionel Messi wa Barcelona kwa aina ya uchezaji.

Anatarajiwa kuanza kucheza katika kikosi B cha Real Madrid chini ya kocha Mfaransa Zinadine Zidane.