Chelsea,Mancity na Totenham nje ya F.A

Haki miliki ya picha PA
Image caption fa

Manchester City,Chelsea Southampton na Totenham zimeondolewa katika mechi za kombe la FA baada ya kuadhibiwa na timu kutoka daraja la chini la ligi ya EPL.

Timu hizo ambazo zinaongoza katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza Zilishangazwa baada ya kushindwa nyumbani na wapinzani wao.

Hii ni mara ya pili kwa mabingwa wa ligi ya Uingereza Mancity kuondolewa nyumbani na Middlesborough ambao walishinda kwa 2-0.

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption fa

Vilevile kilabu ya daraja la kwanza Bradford City ilionyesha mchezo wa hali ya juu ilipotoka nyuma 2-0 na kuweza kuwashinda viongozi wa ligi ya Uingereza Chelsea 4-2 katika mechi ya FA ilioijaa mbwembwe za aina aina.

Katika uwanja wa Totenham bao la Jeffrey Schlupp lilisaidia Leicester kuishinda Totenham.

Leicester ilikuwa nyuma kwa bao moja kabla ya kusawazisha na kuongeza la ushindi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption fa

Uwanjani Southampton Mshambuliaji Marouane Chamakh alifunga mabao mawili na kuisaidia kilabu ya Crystal palace kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya Southampton katika mechi iliokuwa na mchezo mzuri.

Matokeo ya FA

Cardiff 1 - 2 Reading FT

Chelsea 2 - 4 Bradford FT

Derby 2 - 0 Chesterfield FT

Man City 0 - 2 Middlesbrough FT

Preston 1 - 1 Sheff Utd FT

Southampton 2 - 3 Crystal Palace FT

Sunderland 0 - 0 Fulham FT

Tottenham 1 - 2 Leicester FT