Ronaldo:Arsenal ilishindwa kunisajili

Image caption Cristiano Ronaldo

Mchezaji bora wa soka duniani Cristiano Ronaldo alikataa kusajiliwa na kilabu ya Arsenal kwa kuwa bei ya kuujenga uwanja wa Emirates wakati huo uliiwacha kilabu hiyo bila senti.

Mchezaji huyo wa Real Madrid aligunduliwa na The Gunners lakini Manchester United ikamsajili mwaka 2003.

Wakala wa Ronaldo Jorge Mendes amesema kuwa gharama ya uwanja wa Emirates uliondoa fursa ya Arsenal kumsajili mchezaji huyo.

Katika kitabu chake kipya Mendes anasema kuwa kuna wakati ambapo alidhani Ronaldo atajiunga na Arsenal .

''David Dein ni mtu mzuri sana lakini kutokana na kujengwa kwa uwanja wa Emirate ,kilabu hiyo haikuwa na fedha na haikuwezekana kumsajili Ronaldo'',alisema Mendes..