Senegal yatoka sare na Afrika Kusini

Image caption Senegal yaizuia Afrika kusini

Senegal iliwashangaza wengi ilipotoka nyuma na kuizuia Afrika Kusini katika mechi za mataifa ya Afrika kundi la C zinazoendelea Equitorial Guinea.

Baada ya kipindi cha kwanza kukamilika bila timu zote kuona lango la mwengine,Oupa Manyisa alifunga bao la kwanza kunako sekunde 62 za kipindi cha pili na kuiweka Afrika kusini kifua mbele.

Hatahivyo Senegal iliendelea kutafuta bao la kusawazisha huku bao la Sadio Mane likikataliwa kwa kuotea kabla ya Kara Mbodji kufunga kupitia kichwa.

Hatahivyo Simba hao wa Teranga hawajafuzu katika robo fainali huku Afrika kusini ambayo ni ya mwisho katika kundi hilo ikiwa na fursa ya kufuzu iwapo itashinda mechi yake ya mwisho licha ya kuwa na alama moja.