Ronaldo apewa kadi nyekundu kwa kupigana

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ronaldo ampiga Edimar

Mchezaji nyota wa Real Madrid alipewa kadi nyekundi katika mechi dhidi Cordoba baada ya kumpiga mchezaji Edimar.

Ronaldo alipewa kadi hiyo ya adhabu ikiwa imesalia dakika 7 katika mechi ambayo Real Madrid ilipata ushindi wa 2-1.

Baada ya kumpiga teke kutoka nyuma mchezaji Edimar,Ronaldo pia alimzaba kofi.

Haki miliki ya picha getty
Image caption Ronaldo

Ronaldo alinusurika kadi nyekundu awali baada ya kumpiga ngumi mlinzi Jose Angel Crespo wa Cordoba.

Refa hakuona kisa hicho lakini baada ya kutolewa nje kwa mara ya tisa ,mchezaji huyo wa Ureno aliifuta vumbi beji yake aliyopewa kama mchezaji bora duniani huku mashabiki wa upinzani wakimkemea.