Kocha wa Senegal aishtumu West Ham

Haki miliki ya picha BBC Afrique
Image caption Kocha wa Senegal Alain Giresse aishtumu West Ham

Klabu ya West Ham ilionyesha mfano m'baya kwa kumchezesha mshambuliaji Diafra Sakho wikendi iliopita kulingana na kocha wa Senegal Alain Giresse.

Sakho mwenye umri wa miaka 25 alijiondoa katika kikosi cha Senegal cha kombe la mataifa ya Afrika mapema mwezi hutokana na jeraha la mgongo,lakini akaichezea kilabu ya West ham siku ya jumapili.

''Iwapo huwezi kusafiri kwa wiki sita na mara ghafla unacheza soka,basi kuna dawa ya miujiza Uingereza'',alisema Giresse.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Diafra Sakho

''Nimeshangaa kugundua kwamba alicheza .

Sakho alikuwa amechaguliwa katika kikosi cha watu 23 cha timu ya Senegal kabla ya kujiondoa kabla ya michuano ya kombe hilo ilioanza januari 17.