Chelsea kuchuana na Tottenham fainali

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Totenham na Sheffiled

Tottenham ilitoka nyuma na kuishinda kilabu ya ligi ya daraja la kwanza nchini Uingereza Sheffield United na kuweka tarehe na Chelsea katika fainali ya kombe la League Cup mnamo tarehe mosi mwezi Machi.

Hii ni baada ya mchezaji Christian Eriksen kufunga bao la dakika za mwisho.Mkwaju wa adhabu uliopigwa na Ericksen uliifanya Totenham kuwa kifua mbele kwa mabao shinda 2-0.

Hatahivyo mchezaji wa Sheffield mwenye umri wa miaka 18 Che Adam alifunga mabao mawili akiwa karibu na eneo la hatari katika kipindi cha dakika tatu na kuweka matumaini ya mda wa ziada kuongezwa.

Lakini Eriksen alipata bao la ushindi na kufanya mambo kuwa 3-2.

Spurs iliicharaza Chelsea katika fainali ya kombe hilo mwaka 2008 na timu hizo mbili zitakutana tena katika uwanja wa Wembley,siku tatu kabla ya Tottenham kukabiliana na Firentina katika michuano ya kuwania kombe la Yuropa.