Guinea yafuzu, Mali yabeba virago.

Haki miliki ya picha BEHROUZ MEHRIAFP
Image caption Guinea ikicheza dhidi ya Iran katika mechi ya awali

Baada ya droo kufanywa ,Guinea imefuzu katika robo fainali ya kombe la mataifa ya Afrika huku Mali ikibeba virago na kurudi nyumbani.

Mbinu hiyo ilitumiwa kutafuta mshindi wa pili katika kundi hilo baada ya timu hizo kupata alama na mabao sawa.

Guinea sasa itacheza dhidi ya Ghana katika mojawapo ya robo fainali ambayo itafanyika wikendi hii.

Kumekuwa na ukosoaji kutoka kwa makocha wa timu zote mbili za Mali na Guinea kuhusu mbinu inayotumiwa kumpata mshindi.