Mali na Guinea kupigiwa kura

Haki miliki ya picha Associated Press
Image caption Timu ya zamani ya Ivory coast baadhi ya wachezaji wapo kwenye timu ya sasa iliyopo Equatorial Guinea

Ivory Coast imekuwa timu pekee kutoka kundi D kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuifunga Cameroon goli moja kwa nunge.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo kati ya Guinea na Mali imeshindikana kumpata mshindi atakaingia robo fainali baada ya mechi hiyo kumalizika kwa sare ya goli moja kwa moja.

Timu zote mbili Guinea na Mali zote zina pointi sawa ya pointi na magoli matatu ya kufunga.

Kwa sasa timu moja kati ya Guinea au Mali itasonga mbele hatua ya robo fainali baada ya kura itakapigwa hii leo na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF.