Rita Jeptoo apigwa marufuku ya miaka 2

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mwanariadha wa Kenya Rita Jeptoo apigwa marufuku ya miaka miwili kwa kugunduliwa alitumia dawa za kusisimua misuli

Mshindi wa mbio za Boston na Chicago Marathon katika kipindi cha miaka miwili iliopita mkenya Rita Jeptoo amepigwa marufuku katika mchezo huo kwa miaka miwili baada ya kugunduliwa alitumia dawa za kusisimua misuli,shirikisho la riadha nchini Kenya AK limesema.

''AK imefuata maagizo yote katika kisa cha Rita na kwamba ni haki kwa yeye kupewa marufuku ya miaka miwili'',afisa mkuu wa shirikisho hilo Issac Kamande aliwaambia waandishi habari.

Jeptoo amekana kutumia dawa za kusisimua misuli ,akiwaamba wana habari mwaka uliopita kwamba madai hayo dhidi yake ni ya uongo.