Wenger:Paulista hajui kizungu

Image caption Gabriel Paulista

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kwamba kutojua kizungu kwa beki mpya wa timu hiyo Gabriel Paulista huenda kukaifanya timu hiyo kufungwa mabao.

Beki huyo kutoka Brazil atashirikishwa katika mechi dhidi ya Aston Villa siku ya jumapili baada ya kusajiliwa kutoka Villareal kwa kitita cha pauni millioni 11.2.

''Kwa sasa haongei hata neno moja la kizungu,na hiyo inaweza kukufanya ufungwe mabao ''alisema Wenger.

Haki miliki ya picha b
Image caption Paulista

Wenger ameongeza kwamba Gabriel ambaye amekuwa akishirikishwa katika mechi zote za Villareal msimu huu atahitaji mda zaidi ili apate uzoefu katika ligi ya Uingereza.

Kocha huyo pia amesema kuwa mchezaji Francis Coquelin anakaribia kuandikisha mktaba mpya ,lakini nahodha Mikel Arteta bado hajakubali kutia sahihi kandarasi mpya.