Equitorial Guinea yaibamiza Tunisia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption tunisia

Equitorial Guinea iliishinda Tunisia katika mazingira ya kutatanisha ili kufika katika nusu fainali ya kombe la mataifa ya Afrika.

Ahmed Akaichi aliiweka kifua mbele Tunisia na kuweka matumaini ya timu hiyo kufuzu katika nusu fainali alipocheka na wavu kufuatia krosi nzuri iliopigwa na Hamza Mathluthi.

Waandalizi wa dimba hilo wanaoorodheshwa nafasi 96 nyuma ya wapinzani wao walilazimisha mechi hiyo kuchezwa katika dakika za ziada baada ya Javier Balboa kupata bao la penalti katika dakika za lala salama ilipodaiwa kwamba Ali Maaloul alimchezea visivyo Ivan Bolado.

Na Balboa alifunga bao la ushindi baada ya kupiga mkwaju wa adhabu.

Equitorial Guinea itakutana na Ghana ama Guinea katika semi fainali ya kwanza siku ya Alhamisi.