Ghana kupambana na Guinea

Haki miliki ya picha AFP
Image caption ghana

Mlinzi wa Ghana Daniel Amartey amesema kuwa yuko tayari kwa mechi ya leo dhidi ya Guinea

Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 20 na anayechezea kilabu ya Copenhagen alipata jeraha katika mechi dhidi ya Afrika kusini siku ya jummane.

Guinea nayo itamkosa mlinzi Florentin Pogba ambaye ana jeraha la paja na amerudi katika kilabu yake ya Ufaransa St Etienne,huku nahodha Kamil Zayate akiwa bado anakabiliwa na jeraha la mguu.

Ibrahim Traore ambaye ni nahodha msaidizi anatarajiwa kucheza licha ya kutolewa dhidi ya Mali.