Tunisia yasema refa hakutenda haki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Refa akiwapa equitorial Guinea mkwaju wa penalti katika mechi kati ya Tunisia na wenyeji equitorial Guinea

Kocha Goerges Leekens wa Tunisia ameelezea kushindwa kwa kikosi chake na Equitorial Guinea katika mchuano wa kombe la Afrika kama aibu katika soka.

Tunisia ilikuwa inaongoza wakati Equitorial Guinea ilipopewa mkwaju wa penalti katika dakika ya 91 na hivyobasi kupoteza 2-1 wakati wa mda wa ziada katika mechi ya robo fainali.

''Refa wa mechi hiyo alifanya makosa makubwa sana ,si haki'',alisema Leekens.Matokeo yalilazimishwa siwezi kukubali'',.

Tayari afisa mkuu wa soka nchini Tunisia Wadie Jary amejiuzulu katika shirikisho la soka barani Afrika CAF ili kupinga yaliotokea.

Haki miliki ya picha
Image caption kikosi cha Tunisia

Leekens aliongeza:''Katika miaka yote 45 ya soka nikiwa mchezaji kwa kipindi cha miaka 15 na miaka 30 kama mkufunzi sijaona tukio kama hili''.

''Matokeo yalilazimishwa,na siwezi kukubali''.

Ilikuwa uamuzi mkali baada ya refa wa Mauritania Rajindraparsad Seechur kuonyesha eneo la kupiga penalti katika mda wa lala salama,akiseama kuwa Ali Maloul alimchezea visivyo Ivan Bolado.