Nchi nne kuwasili Tanzania kwa Kriketi

Image caption Timu ya Kriketi

Timu kutoka Namibia, Nigeria, Botswana, Kenya na Uganda zitawasili Tanzania wikiendi hii kwa ajili ya michuano ya ICC-Africa ya kriketi kwa wanaume chini ya miaka 19 itakayoanza mapema Jumatatu ijayo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa afisa wa chama cha kriketi Tanzania (TCA), Kazim Nasser, timu hizo zitawasili sambamba na ujio wa marefa (umpires) na kamishina wa mashindano kutoka nchini Afrika ya Kusini.

Michuano hiyo itakuwa ni sehemu ya kufuzu kwa ajili ya kombe la dunia litakalofanyika mwakani Bangladesh.

Nasser amesema wakiwa kama wenyeji, wamejipanga vizuri kwa ajili ya mashindano hayo yatakayodumu kwa muda wa juma moja.

Dar es Salaam Gymkhana Club, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Annadil Burhani ndivyo viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano hiyo mikubwa Afrika.

Tanzania imefanikiwa kupata nafasi ya kushiriki baada ya kuwa mabingwa wa michuani hiyo ya ligi daraja la pili iliyofanyika Lusaka, Zambia mwaka jana.