FA: Man United kuivaa Cambridge United

Haki miliki ya picha
Image caption Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal

Manchester United itashuka dimbani kuikabili timu ya Cambridge United katika mchezo wa marudio kombe la FA.

baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa kwanza uliochezwa Abbey Stadium Nyumbani kwa Timu hiyo ya Daraja la Chini, Ligi daraja la 2.

Hii ni Mechi ya raundi ya 4 ya FA Cup na Mshindi atatinga Raundi ya 5 na kucheza na Mshindi kati ya Preston au Sheffield United ambao nao wanarudiana leo Jumanne.

Mechi za Raundi ya 5 zitachezwa Wikiendi ya Februari 14 na 15.

Michezo mingine inayochezwa leo ni Fulham dhidi ya Sunderland, huku Sheffield United wakiwakabili Preston

Jumatano kutakua na mchezo mmoja ambapo majogoo wa jiji Liverpool watakua wakichuana na Bolton Wanderers.