Harry Redknapp ajiuzulu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Harry Redknapp

Harry Redknapp amejiuzulu kazi ya kuifundisha timu ya Queens Park Rangers ya ligi kuu ya England,EPL.

Redknapp alimpigia simu mmiliki wa timu hiyo Tony Fernandes, siku ya Jumanne akimweleza kujiuzulu kazi hiyo ya ukocha kutokana na sababu za kiafya.

Saa chache baada ya muda uliowekwa kumalizika, Redknapp alikuwa akimwaambia mtu ambaye alijenga imani kwake kama wiki mbili zilizopita kuwa kazi hiyo sasa basi.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 67-alielezea matatizo yake ya kiafya kutokana na goti alilofanyiwa upasuaji kama sababu ya kuondoka kwake katika kazi hiyo lakini alionekana kuwa na thamani ndogo kwa kushindwa kuikwamua timu kutoka nafasi ya 19 iliyopo katika msimamo wa timu 20 za ligi kuu ya England.