Uhamisho wa Adebayor wakataliwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Emmanuel Adebayor

Daniel Levy aliingilia kati ili kusitisha uhamisho wa mshambuliaji nyota Emmanuel Adebayor aliyetaka kujiunga na West Ham kutoka Tottenham katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho.

Mwenyekiti huyo wa Tottenham alipinga mpango wa West Ham wa kumnunua mchezaji huyo baada ya mshambuliaji huyo wa Togo mwenye umri wa miaka 30 kukubali masharti yote.

Tottenham ilikuwa tayari kumruhusu mchezaji huyo kuondoka na walikuwa tayari kugharamia nusu ya pauni laki moja kama marupuru yake ya kila wiki .

Lakini walikataa masharti hayo kwa kuwa West Ham ni wapinzani wao wa moja kwa moja.