Ligi kuu England kuendelea wikiendi hii

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Shughuli pevu wikiendi hii Ligi kuu England

Ligi Kuu England itaendelea tena wikiendi hii ambapo michezo saba ya mzungo wa raundi ya 24 itapigwa katika viwanja tofauti.

katika uwanja wa White Hart Lane, Tottenham wataikaribisha Arsenal kwenye Dabi ya London ya Kaskazini, Arsenal wako nafasi ya tano wakiwa na pointi 42 huku Tottenham wakiwa nafasi ya sita kwa pointi 40.

Alexis Sanchez atakosa mchezo huu kutokana na kuwa majeruhi huku mshambuliaji Dany Welback atakua anarejea baada ya kuwa nje ya uwanja toka mwezi Desemba.

Vinara wa ligi hiyo Chelsea watashuka dimbani kuwakabili Aston Villa huku timu hiyo ikiendelea kukosa huduma za mshambuliaji wake Diego Costa.

Man City walioko nafasi ya pili kwa alama 48 alama 5 nyuma ya vinara Chelsea wao watakua na kibarua cha kuwania alama tatu muhimu kwa kuwakabili Hull city.

Majongoo wa jiji Liverpool watachuana na wapinzani wao wakubwa Everton katika kuwania pointi tatu muhimu.

Michezo mingine itakua ni kati ya timu inayoburuza mkia Leicester City dhidi ya Crystal Palace, huku QPR wakishuka dimbani kuwakabili Southampton

Mchezo wa mwisho wa ligi hiyo kwa siku ya jumamosi utakua ni kati ya Swansea na Sunderland