Guinea ya Ikweta yatozwa Faini na CAF

Haki miliki ya picha
Image caption Polisi ililazimika kutumia nguvu kutuliza ghasia uwanjani

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeiadhibu nchi ya Guinea ya Ikweta baada ya mashabiki wake kufanya vurugu katika mchezo wa nusu fainali.

Guinea ya Ikweta inatakiwa kulipa faini ya pauni 65,000 (US$100,000) kwa vurugu zilizofanywa na Mashabiki wake na kusababisha mchezo wa nusu fainali kati yao na Ghana kusimama kwa muda.

Pia watatakiwa kuwahudumia mashabiki 36 waliopata majeruha katika vurugu hizo