AFCON:Usalama waimarishwa katika fainali

Haki miliki ya picha afp
Image caption maafisa wa polisi wakiweka usalama

Usalama umeimarishwa kwa mechi ya fainali ya kombe la Afrika kati ya Ivory Coast na Ghana .

Ghasia zilizosababishwa zilizuka wakati wa nusu fainali ya pili kati ya Ghana na waandalizi Equitorial Guinea,baada ya mashabiki wa nyumbani kurusha vitu ndani ya uwanja.

Mechi ya leo inaanza saa nne usiku ikitarajiwa kuwa marejeleo ya fainali ya mwaka 1992, ambapo Ivory Coast ilishinda kupitia mikwaju ya penalti na kuwezesha kushinda kwa mara ya kwanza kombe hilo la mataifa ya Afrika.

Ghana imeshinda kombe hilo mara nne .

Katika mechi ya kumtafuta mshinda wa tatu siku ya jumamosi DR Congo iliishinda Equitorial Guinea 4-2 kupitia mikwaju ya penalti katika mechi ambayo haikukumbwa na ghasia zozote.