Real Madrid yasakamwa 4-0 na Atletico

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Cristiano Ronaldo ashangaa baada ya kucharazwa mabao 4-0 na Atletico Madrid

Viongozi wa ligi ya La Liga Real Madrid siku ya jumamosi waliona cha mtema kuni waliposakamwa mabao 4 bila jibu na wapinzani wao Atletico Madrid katika mechi ya Derby iliochezwa katika uwanja wa Vincente Calderon.

Real iliokuwa ikiuguza majeraha mengi ililazimika kutaja mabeki m'badala katika mechi yao ya ugenini.

Hatahivyo mabeki hao hawakuweza kuhimili kishindo cha mashambulizi ya mabingwa wa ligi Atletico Madrid.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ateltico madrid

Mabao ya haraka yaliofungwa na Tiago,Saul Niguez yaliiweka Atletico kifua mbele katika kipindi cha kwanza,kabla ya mabao mengine mawili yaliofungwa katika kipindi cha pili na Antoine Griezman na Mario Mandzukic kupiga msumari wa matumaini ya Real.

Baadaye wachezaji pamoja na mashabiki wa Atletico walisherehekea sana ushindi huo.