Sam Smith ashinda tuzo Marekani

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sam Smith mshindi wa tuzo za Grammys

Mwanamuziki raia wa Uingereza Sam Smith ameshinda tuzo mbili za Grammys zilizofanyika Los Angles Marekani.

Smith ametangazwa mshindi wa kwanza ambapo kupitia wimbo wake wa In The Lonely Hour ulimfanya aibuke mshinndi wa miondoko ya Pop Vocal Album.

Smith alikuwa mmoja wa wanamuziki walikuwemo katika orodha ya kuwania tuzo hizo.Shairi lake la Stay With Me lilimfanya mwanamuziki huyo kuibuka mshindi wa kimataifa mwakajana.

Beyonce na Pharrell Williams ni miongoni mwa wanamuziki wengine waliokuwa wameteuliwa kuwania tuzo hizo kwa kigezo namba sita.

Hta hivyo Pharrell Williams yeye aliibuka mshindi wa maonesho ya miondoko ya Pop Solo Performance kwa kibao chake Happy, Beyonce naye akajinyakulia ushindi wa R&B kupitia kibao Drunk In Love ambao alimshirikisha mume wake Jay Z.