Azam kukwea kilele cha ligi Tanzania?

Image caption John Boko akishangilia kwa namna yake.

Ligi ya kuu ya Tanzania itaendelea tena leo kwa timu ya Azam FC Ikiwakaribisha Mtibwa Sugar mchezo utakaopigwa katika dimba la Azam Complex

Kikosi cha Azam kinahitaji ushindi katika mechi hiyo ili kirejee kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 25 sawa na vinara wa sasa, Yanga SC.

Mtibwa Sugar itaingia Uwanjani ikisaka ushindi wake wa kwanza baada ya kucheza mechi saba bila ushindi ikitoka sare mara tano na kupoteza mechi mbili.

Timu ya Mtibwa haina historia nzuri inapokutana na Azam FC, watakua wanahitaji kupata ushindi ili kurejesha morari ya timu baada ya kupoteza mweleke siku za karibuni baada ya kuongoza ligi kwa muda mrefu.