Pearson: Leicester hawanifukuzi ng'o

Image caption Nigel na dole gumba juu kwa kujiamini.

Meneja wa timu ya Leicester Nigel Pearson amesema klabu hiyo haina mpango wa kumfukuza pamoja na taarifa zilizo sambamba kuwa atatimuliwa.

Nigel Pearson mwenye miaka 51 aliendelea kushudia timu yake ikipokea kichapo cha bao 2-1 dhidi ya Arsenal.

"Wamiliki hawana mpango wa kunifukuza, bado nina mahusiano mazuri na wamiliki."

Kocha huyu anakibarua kizito cha kuinasua toka mkiani timu yake amabyo haina mwenendo mzuri katika ligi.

Leicester City wanaburuza mkia wa ligi ya England wakiwa na alama 17 baada ya kushuka dimbani mara 25.