Barcelona yam'mezea mate Alexi Sanchez

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Barcelona yammezea mate mchezaji Alexi sanchez wa Arsenal

Afisa mpya anayesimamia maswala ya uhamisho wa wachezaji katika kilabu ya Barcelona amesema kuwa ana hamu ya kumsajili tena mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez.

Sanchez aliuziwa Arsenal katika msimu wa kiangazi kwa kitita cha takriban pauni millioni 30 na hadi wakati huo ameonyesha umahiri wake katika ligi ya Uingereza.

Barcelona kwa sasa inahudumia marufuku ya kutosajili ambayo inaendelea hadi mwishoni mwa msimu huu,hatua inayomaanisha kwamba haiwezi kusajili mchezaji mwengine yeyote.

Sanchez amefunga mabao 18 katika mechi 32 na majarida ya michezo nchini Uhispania yameshtumu hatua ya Barcelona kumwachilia mchezaji huo.

Lakini katika mwelekeo mpya ,afisa mpya anayehusika na maswala ya uhamisho wa wachezaji Ariedo Braida amesema angetaka kumsajili tena Sanchez ili kurudi katika uga wa Nou Camp.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mchezaji Alexi Sanchez

''Ningependa kumsajili Sancheza katika kilabu yoyote niliopo''.

''Namjua sana lakini sijui ni sababu gani zilizosababisha kilabu hii kumwachilia,na sasa mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji wazuri katika ligi ya Uingereza na ari yake iko juu''.

Tayari Arsenal inadaiwa kutafuta sahihi ya Sanchez ili kumuweka katika kilabu hiyo kwa mda mrefu zaidi.