Chelsea yashtumiwa kwa kumshawishi refa

Image caption Wachezaji wa Chelsea

Mkufunzi wa timu ya Everton Robert Mertinez amewashtumu wachezaji wa Chelsea kwa kujaribu kumshawishi refa katika mechi iliotawaliwa na hasira nyingi kutoka kwa wachezaji wote ambapo Chelsea ililazimika kufunga bao la dakika za mwisho ili kuilaza Everton 1-0 uwanjani darajani.

Bao la dakika za lala salama la Willian liliwekwa wavuni baada ya Gareth Barry kupewa kadi nyekundu huku ugomvi ukizuka baada ya Branislav Ivanovic kumchezea visivyo James McCarthy wa Everton tukio ambalo lilikwepa adhabu ya refa.

''Ni wazi kwamba kile wachezaji wa Chelsea walijaribu kufanya ni kumshawishi refa'',Martinez aliiambia BBC.

Mourinho alikatiza mahojiano yake na BBC wakati alipoulizwa kuhusu nidhamu ya wachezaji wa Chelsea.

Mechi iliokuwa iende sare iliimarika katika dakika za mwisho baada ya Gareth Barry kupewa kadi ya pili ya njano kwa kumuangusha Willian.

Huku wachezaji wa pande zote mbili wakikabiliana, Ivanovich alimkaba koo Mc Carthy na kuonekana akitaka kumpiga kichwa kiungo huyo wa kati wa Everton.