Je wajua mbwa ana jua tofauti zetu?

Image caption Mbwa rafiki

Utafiti unaonesha kwamba watu wanaopenda wanyama hasa mbwa,utafiti unaanisha kuwa binadamu hawezi kuficha hisia zake kwa mbwa ,kwani mnyama huyo anao uwezo mkubwa wa kushuku mambo na tofauti zetu kati ya furaha na taswira yenye hasira.

Wanasayansi wanaofanya utafiti katika kitengo cha Messerli Research Institute , juu ya maabara ya mbwa wenye utambuzi ,mjini Vienna huwafundisha mbwa kung’amua picha mbalimbali ikiwa picha aionayo ni ya mtu mwenye furaha ama hasira .

Katika utafiti uliofanywa mfululizo,wanasayansi walionesha mbwa taswira za watu ambazo hawakuwahi kuziona katika mafunzo yao, kumtambua mbwa kama anaweza kugundua sura na muonekano tofauti kwenye picha hizo.

Utafiti huu,ambao ulichapishwa katika jarida la masuala ya biolojia,ni sehemu ya utafiti mkubwa kujifunza namna rafiki wa mwanadamu ‘MBWA’ wanavyoweza kuchangamana.

Lengo kubwa la utafiti huo ni juu ya swali kubwa la mawasiliano yao, anasema kiongozi wa utafiti huo Profesa Ludwig Huber .Inakuwaje mbwa ajiungamanishe na mwanadamu kwa kiasi hiki? Na nini hutokea wakati wa mchakato wa ndani?

Wanasayansi wamerudia mara ishirini kuwaonesha mbwa nusu picha, ama iwe mdomo wa chini ama sehemu ya juu ya jicho la mtu mwenye furaha ama uso wenye hasira,lakini mbwa waling’amua tofauti.