Steven Gerrard Kufanyiwa vipimo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Steven Gerrard

Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard kufanyiwa vipimo vya kuchunguza jeraha la nyama za paja alilolipata wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Tottenham.

Kuna mashaka makubwa kiungo huyo atakosa mchezoo wa raundi ya tano ya kombe la FA watakaocheza na Crystal Palace.

Kuumia kwa Gerrard ni pigo kwa kikosi cha Brendan Rodgers baada ya kiungo mwingie

Lucas Leiva kuumia katika mchezo huo .

"Kwa bahati mbaya, alijisikia maumivu ya nyama za paja na kuendelea na mchezo mpaka mwisho,tunasubiri majibu baada ya vipomo vya daktari," alieleza kocha msaidizi wa liverpool Colin Pascoe.

Pia mshambuliaji Sterling Raheem ambae ana maumivu ya mguu yaliyopelekea kukosa dhidi ya Tottenham anaendelea vizuri na anatarajiwa kurudi dimbani wikiendi ijayo.