Liverpool yafuzu robo fainali ya FA

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Danniel Sturidge akifunga bao lake

Mabingwa mara saba Liverpool walitoka nyuma na kuishinda Crystal Palace na kufuzu katika robo fainali ya kombe la FA.

Fraizer Campbell alikuwa ameiweka kifua mbele Crystal Palace baada ya kichwa cha Dwight Gayle kupanguliwa na kipa wa Liverpool Simon Mignolet.

Lakini Danniel Sturridge alisawazisha baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Jordan Henderson.

Adam Lallana alifunga bao la ushindi kutoka pasi iliopigwa na Mario Balotelli.