Susie Wolff kujaribu Magari ya Williams F1

Haki miliki ya picha PA
Image caption Dereva Susie Wollf

Dereva Susie Wolff anatarajia kufanya majaribio ya magari ya Williams FW37 huko Circuit de Catalunya.

Wolff mwenye miaka 32 aliteuliwa kuwa dereva wa kuifanya majaribio mwezi November mwaka jana baada ya kushiriki mara mbili katika msimu uliopita.

Dereva huyu atafanya majaribio ya magari haya siku ya kwanza ya majaribio,Huku maderevaValtteri Bottas na Felipe Massa watatumia siku na nusu katika siku tatu za majaribio.

Bottas ataanza kuendesha siku ya ijumaa kabla ya Massa kufanya hivyo jumamosi

Baada ya kupewa jukumu hilo la kuanza kujaribu magri dereva huyu mwanamke alisema “michuano ya F1 sio dunia ya wanaume"