Nahodha wa Guinea ya Ikweta atundika daruga

Image caption Nahodha mstaafu Juvenal Owono

Nahodha wa timu ya taifa ya Guinea ya ikweta Juvenal Edjogo Owono Montalban amestaafu kucheza soka la kimataifa.

Nyota huyu mwenye miaka 35 amestaafu baada ya kuwakilisha nchi yake kwenye michuano ya kombe la afrika.

“Baada ya miaka kumi na mbili ya kuitetea rangi ya nchi yangu,natangaza nimeamliza muda wangu wa kuitumika timu ya taifa ilikua ni muhimu kuchezea timu katika kipindi changu cha uchezaji ni muda wa kuachia njia kwa wachezaji vijana kucheza”.

Juvenali ameichezea timu ya taifa jumla ya michezo 67 akianza mechi 62 katika timu ya taifa.