Michauno ya vijana Kriket yashika kasi

Image caption Timu ya mpira wa magongo wakishangilia kiaina

Michuano ya kriket kwa vijana chini ya umri wa miaka 19 kuendela kutimua vumbi Jijin Dar es Salaam Tanzania.

Baada kuwa mapumziko kwa siku ya jana leo Namibia watachuana na timu ya Uganda katika mchezo utakaochezwa kwenye viwanja vya Gymkhana.

Wenyeji wa michuano hii Tanzania watakua na kibarua kigumu dhidi ya kikosi cha timu ya Nigeria mchezo utakaochezwa kwenye viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Mchezo wa mwisho utawakutanisha Botswana na Kenya ambapo mchezo huu utachezwa kwenye uwanja wa Anadil Burhani.

Namibia ndio wanaongoza michuano hii wakiwa na alama 6 na mikimbio 759 wakifuatiwa na Uganda wenye alama 4 wakiwa na mikimbio 293.

Bigwa wa michuano hii atakwenda kushiriki michuano ya kombe la dunia kwa vijana itakayofanyika Bangladeshi februari mwakani.