Kriketi: Zimbabwe yailaza UAE

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kriketi: Zimbabwe yailaza UAE

Zimbabwe ilijirukuta na kusajili mikimbio mingi zaidi katika historia ya kombe la dunia la Kriketi tangu mwaka wa 96 ilipotoka nyuma na kuibana

Miliki za kiarabu katika mechi ngumu ya kombe la dunia ya kundi BA inayoendelea huko New Zealand na Australia.

Mchezaji wa Shaiman Anwar alisajili mikimbio 67 na kuwaongoza UAE kuandikisha mikimbio 285- baada ya kuwapoteza wachezaji 7,

hiyo ikiwa ni idadi kubwa zaidi katika historia ya mashindano ya kimataifa ya kriketi ya siku moja tangu 1996.

Hata hivyo Zimbabwe ilijifurukuta Sean Williams akisajili mikimbio 76 na kuwaongoza watoto wa Mugabe kuandikisha ushindi mkubwa wa Wiketi 4 wakiwa na mipira 12 ya ziada.

Zimbabwe ambayo ilishindwa katika mechi yao ya kwanza dhidi ya Afrika Kusini ilikuwa inahitaji kushinda mechi hii kwa udi na uvumba.